AZAM FC 0-1 YANGA SC: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL – 29/04/2019) Cricketinbuz

AZAM FC 0-1 YANGA SC: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL – 29/04/2019)

AZAM FC 0-1 YANGA SC: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL – 29/04/2019) Detail

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC wamepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC, mchezo ukipigwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Goli pekee la ushindi kwa Yanga limefungwa na Mrisho Ngasa dakika ya 13 akimalizia pasi ya Ibrahim Ajibu baada ya mabeki wa Azam kushindwa kujipanga sawasawa.

Licha ya Azam FC kujibu kwa kufanya mashambulizi mengi hasa kipindi cha pili, haikuweza kusawazisha bao hilo huku ikipoteza nafasi kadhaa za wazi ikiwemo ya dakika ya 84 kupitia kwa Danny Lyanga akiwa uso kwa uso na golikipa.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga iendelee kujikita kileleni ikifikisha pointi 77 juu ya Simba wenye pointi 69 na Azam wamebaki nafasi ya tatu na pointi zao 66.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.